Kanda ya ngono:Djibrill Cisse mashakani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Djibril Cisse

Aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa Djibril Cisse, mwenye umri wa miaka 34, amekamatwa na maafisa wa polisi ili kuchunguzwa kwa madai ya kanda moja ya video kuhusu ngono.

Maafisa wa polisi wa Ufaransa walithibitisha kwamba wanachunguza jaribio la kumhonga mchezaji mwengine wa soka.

Cisse ni miongoni mwa watu wanne waliokamatwa ,kiongozi wa mashtaka wa Ufaransa alithibitisha.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland na QPR alihojiwa kwa kuwa anawajua wachezaji wengine waliohusika kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Mwathiriwa hajatambulishwa na mamlaka kwa kuheshimu hali yake ya faragha.

Cisse alijiunga na Liverpool mwaka 2004 na kufunga mabao 24 katika mechi 74 alizocheza kwa kilabu hiyo ya Mersyside.