Federer atupwa nje michuano ya Shanghai

Image caption Federer ametupwa nje baada ya kuadhibiwa na Albert Ramos-Vinolas

Nyota wa mchezo wa tenesi Roger Federer, ametupwa nje ya michuano ya Shanghai Masters.

Federer anayeshikilia nafasi ya tatu kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume amechapwa na Albert Ramos-Vinolas, anayeshika nafasi ya 70 kwa seti 7-6 2-6 6-3.

Nyota huyo wa tenesi ambaye alikuwa bingwa mtetezi alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza toka alivyopoteza mchezo wa fainali katika michuano ya US Open, dhidi ya Novak Djokovic,

Ramos-Vinolas, ambae amewahi kutwaa mara moja Grand Slam katika misimu mitatu iliyopita hajawahi mfunga mpinzani yeyote aliyeko kwenye nafasi kumi za juu kwa ubora.

Raia huyu wa Hispania atachuana na Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga au Victor Estrella Burgos katika mchezo unaofuata.