Sunderland yazindua kituo cha michezo TZ

Image caption Ukumbi wa michezo

Klabu ya soka ya Sunderland ya Uingereza imeandikisha historia katika sekta ya michezo barani Afrika na hasa katika nchi ya Tanzania baada ya kufungua kituo cha hifadhi ya michezo kwa vijana wadogo katika eneo la kidongo chekundu Jijini Dar es saalam.

Image caption Ukumbi wa michezo

Kituo hicho kitatoa huduma za kimichezo, kielimu na afya kwa wanamichezo chipukizi wanaochipukia nchini Tanzania.

Timu ya Sunderland imeshirikana na kampuni ya kuzalisha umeme ya Marekani ya (Symbion Power) kutengeza sehemu hiyo ya michezo inayoitwa Jakaya Mrisho Kikwete Youth jina la Rais wa Tanzania .

Image caption Ukumbi wa Michezo

Mkurugenzi wa Sunderland Margaret Byrne, ameiambia BBC wanatarajia kituo hicho cha michezo kitawasaidia wanamichezo wachanga wa kizazi cha sasa kuendeleza vipaji vyao.

Kituo hicho kina viwanja vitatu vya nyasi bandia, kiwanja kimoja cha mchanga, viwanja viwili vya mchezo wa mpira wa kikapu, huku kukiwa na taa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya michezo ya usiku.

Image caption Ukumbi wa Michezo

Uzinduzi wa hifadhi hiyo ya michezo ni mpango ulipo kati klabu hii ambayo pia inafahamika kama Black Cats na bara la Afrika katika kufundisha makocha, wachezaji wadogo na kuzijengea uwezo timu za barani Afrika.

Mahusiano ya klabu hii na bara la Afrika yalianza mwaka 2012 walipopata udhamini wa kampuni ya mafuta ya Tullow.

Image caption Ukumbi wa Michezo

Sehemu ya makubaliano ya mkataba huu ilikua ni kuitangaza Afrika ambapo jezi ziliandikwa "wekeza Afrika" na huu ndio utafauti wa klabu hii na vilabu vingine vya ligi ya England vinavyowekeza katika nchi za China na Marekani.

Image caption Ukumbi wa michezo

Kuna watu zaidi ya milioni 200 kutoka ukanda wa jangwa la Sahara, wanafuatilia ligi kuu ya England.

Pamoja na kutokua timu maarufu sana barani humu lakini timu hii inaendeleza miradi ya kijamii katika nchi za Ghana, Zambia, Afrika

Image caption ukumbi wa michezo

Kusini na Tanzania kusaidia kufundisha mpira katika ngazi ya chini.