Djokovic ambwaga Jo-Tsonga,Tenis

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mcheza Tennis,Novac Djokovic

Mcheza Tenis wa Serbia Novac Djokovic amefanikiwa kumshinda Jo-Wilfred Tsonga kwenye fainali za shanghai.

Djokovic amedhihirisha kuwa bado yeye ni mchezaji namba moja Duniani baada ya kutawala katika mchezo dhdi ya mpinzani wake na kumshinda. Msebia huyo alionyesha mchezo wa hali ya juu na kushinda seti 6,2 6,4 ndani ya dakika 78 za mchezo katika uwanja wa Qi Zhong. Djokovic mpaka sasa ameshinda seti 22 na hajafungwa katika mechi 17 alizocheza na hiyo ni rekodi yake tangu kuanza kwa mashindano ya wazi ya US. Mpaka sasa ameshinda mataji 25 moja zaidi Rogger Federa na mawili pungufu dhidi ya anayeshikilia rekodi Rafael Nadal.