Mimi si malaika, Diego Costa asema

Diego Costa Haki miliki ya picha PA
Image caption Costa amepigwa marufuku kucheza mara mbili msimu huu

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amesema anajua kwamba yeye “si malaika” uwanjani na kwamba hatabadilisha mtindo wake wa uchezaji soka.

Costa amepigwa marufuku mechi tatu mara mbili mwaka huu, mara ya kwanza kwa kumkanyaga mchezaji wa Liverpool Emre Can na mara ya pili kwa kumsukuma difenda wa Arsenal Laurent Koscielny.

"Nimefika mbali hivi kutokana na jinsi ninavyocheza,” mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameambia wanahabari wa BBC wa Football Focus.

Costa alizaliwa Brazil lakini huchezea timi ya taifa ya Uhispania.

"Sitabadilisha hilo eti kwa sababu ya vile watu wanachukulia uchezaji wangu.”

Klabu yake ya Chelsea, ambayo imekuwa ikiandikisha matokeo mabaya msimu huu, itakutana na West Ham leo katika Ligi ya Premia.