Hamilton atwaa taji la tatu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lewis Hamilton akichuana kwenye mahindano ya United States Grand Prix

Dereva wa magari yaendayo kasi ya Fomula 1 Lewis Hamilton ameendelea kung'ara msimu huu baada ya kutwaa taji katika michuano ya United States Grand Prix,

Nyota huyo ametwaa hilo la michuano ya dunia na kuwa taji lake la tatu kwa msimu huu wa michuano ya Fomula 1.

Hamilton dereva wa timu ya Mercedes, anakua mwingereza wa pili baada ya Sir Jackie Stewart, kutwaa matatu katika mbio hizo za magari.

Dereva wa timu ya Ferrari Sebastian Vettel, alimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya dereva Nico Rosberg dereva wa timu ya Mercedes.