7 kugombea kiti cha urais wa FIFA

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wagombea 7 watawania tikiti ya kuwa rais wa FIFA.

Wagombea 7 watawania tikiti ya kuwa rais wa FIFA.

Shirikisho hilo lenye makao yake makuu huko Uswisi imethibitisha kuwa wagombea 7 wamewasilisha maombi ya kurithi kiti kitakachowachwa wazi na kuondoka kwa Sepp Blatter.

Uchaguzi wenyewe umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Februari mwakani.

Blatter ambaye hivi sasa anatumikia marufuku ya siku 90 kwa tuhuma za ulaji rushwa na ubadhirifu ameahidi kujiuzulu baada ya shirikisho hilo maarufu duniani kusakamwa na tuhuma za hongo ulaji rushwa na ufisadi.

Prince Ali bin al-Hussein, Musa Bility, Jerome Champagne, Gianni Infantino, Michel Platini, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa naTokyo Sexwale.

Mchezaji wa zamani wa Trinidad David Nakhid hakujumuisha katika orodha hiyo.