Yanga yatoka sare,Simba yapeta

Image caption Kikosi cha Simba ya Tanzania

Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea kutimua vumbi katika viwanja Sita ambapo mabingwa watetezi ligi hiyo Yanga ikiwa ugenini huko Shinyanga ilikwenda sare ya mabao 2-2 na Mwadui Fc.

Wekundu wa msimbazi wakicheza katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wagosi wa kaya Coastal Union

Toto African ikawatambia timu ya Mgambao Shooting kwa kuwachapa kwa bao 1-0, huku wakata miwa wa Mtibwa Sugar wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wakata miwa wenzao wa Kagera Sugar.

Mbeya City wakicheza katika uwanja wao wa Sokoine wakaenda sare ya 1-1 na Majimaji, nao Ndanda wakiwa katika uwanja wao wa Nangwanda sijaona walienda sare ya bila kufungana na Stand United