Refarii aliyekataa kutoa penalti afungiwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu ya soka ya Trabzonspor iliamuru refarii huyo azuiliwe kwa saa kadhaa baada ya kuwanyima penalti dhidi ya mahasimu wao wa jadi Gaziantepspor.

Refarii mmoja na wasaidizi wake walijipata taabani baada ya kufungiwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo na maafisa wa timu moja iliyohisi kuonewa na umamuzi wake.

Timu ya soka ya Trabzonspor iliamuru refarii huyo azuiliwe kwa saa kadhaa baada ya kuwanyima penalti dhidi ya mahasimu wao wa jadi Gaziantepspor.

Cagatay Sahan alifungiwa ndani ya uwanja wa Trabzonspor nchini Uturuki muda mchache tu baada ya kuamua dhidi ya kupeana penalti katika mechi iliyoishia sare ya mabao 2-2.

Haki miliki ya picha thenff
Image caption Cagatay Sahan alifungiwa ndani ya uwanja wa Trabzonspor nchini Uturuki

Inadaiwa kuwa viongozi wa klabu hiyo ya Trabzonspor walihisi Sahan aliwanyima fursa ya kuibuka washindi dhidi ya Gaziantepspor alipoamua kuwa tukio hilo la kuangushwa kwa mchezaji wao katika muda wa mwisho mwisho wa mechi hiyo haikustahili adhabu ya mkwaju wa penalti.

Uamuzi huo hata hivyo uliwaudhi sana mashabiki wa timu ya nyumbani Trabzonspor waliokamia kumpa kichapo cha mbwa .

Rais wa klabu hiyo Ibrahim Haciosmanoglu aliamrisha wafungiwe ndani ya chumba kimoja uwanjani humo.

Haki miliki ya picha hurriyet.com.tr
Image caption Rais wa klabu hiyo Ibrahim Haciosmanoglu aliamrisha wafungiwe ndani

Haciosmanoglu inadaiwa kuwa aliwaruhusu kuondoka baada ya kuzungumza na rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.

Shirikisho la soka la Uturuki limeanzisha uchunguzi kubaini haswa nini kilichoendelea na kusababisha hatua kama hiyo kuchukuliwa.