Mkenya kuendesha baiskeli Cairo hadi Cape Town

Image caption Kinja na wenzake wanapanga kuvunja rekodi ya dunia

Mwendeshaji baiskeli mashuhuri kutoka Kenya David Kinja akishirikiana na waendeshaji baiskeli wengine watatu anashiriki jaribio la kutaka kuvunja rekodi ya uendeshaji baiskeli duniani.

Wanne hao wanaendesha baiskeli kutoka Cairo hadi Cape Town.

Tayari wamfika Kenya na sasa wanapanga kupitia Tanzania, Zambia, Botswana kabla ya kumalizia safari Afrika Kusini.

Walianza safari yao Oktoba 9 na lengo lao ni kumaliza safari hiyo yenye urefu wa kilomita 10,600 katika chini ya siku 34.

Mwingereza Mark Beaumont anashikilia rekodi ya sasa baada yake kutumia siku 41, saa 10 na dakika 22 kumaliza safari hiyo.

Kinja anashirikiana na kiongozi wa kundi Nicholas Bourne kutoka Uingereza, Mark Blewett kutoka Afrika Kusini na David Martin kutoka Zimbabwe.