Urusi imekana kuwa ilipendelewa na FIFA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi imekana kuwa ilipendelewa na FIFA

Urusi imekana kuwa ilipendelewa wakati kamati kuu ya FIFA ilipokutana kutoa zabuni ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018.

Maafisa wa shirikisho la soka la Urusi wamekana kuwa walifahamu kuwa taifa lao lilikuwa limependelewa na shirikisho la soka duniani FIFA hata kabla ya kura hizo kupigwa.

Mkurugenzi mkuu wa kamati andalizi ya michezo hiyo Alexei Sorokin,alisema kuwa Urusi ilikuwa imetekeleza kikamilifu matakwa na vigezo vyote vilivyowekwa kwa ajaili ya nchi mwenyeji wa fainali za kombe la dunia la mwaka wa 2018.

Bwana Sorokin anasema kuwa Urusi haikushinda kwa sababu ilipendelewa na mtu yeyote.

Bali Urusi ilishinda kutokana na kuwa ilitoa mpango bora zaidi ya washindani wake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkurugenzi mkuu wa kamati andalizi ya michezo hiyo Alexei Sorokin,alisema kuwa Urusi ilikuwa imetekeleza kikamilifu matakwa na vigezo vyote

Waziri wa michezo wa Urusi,Vitaliy Mutko amemtetea rais huyo wa FIFA aliyepigwa marufuku na kamati maalum ya maadili akisema kuwa matamshi yake yamepokelewa na kutafsiriwa visivyo.

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA alinukuliwa akisema kuwa wanakamati wa shirikisho hilo walijadiliana hata kabla ya kupigwa kura ya kutoa zabuni ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 katika kikao cha faragha huko Afrika Kusini mwaka wa 2010.