Chelsea walazwa, Arsenal na Man City washinda

Masaibu ya Chelsea yaliendelea Jumamosi baada yao kulazwa 3-1 na Liverpool uwanjani Stamford Bridge, Arsenal na Manchester City walipata ushindi.

Ushindi wa Liverpool unaongeza shinikizo kwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho ambaye klabu yake imeshindwa kabisa kutamba msimu huu.

Matokeo kamili ya mechi za Jumamosi ni kama ifuatavyo:

Chelsea 1-3 Liverpool

Crystal Palace 0-0 Man Utd

Man City 2-1 Norwich

Newcastle 0-0 Stoke

Swansea 0-3 Arsenal

Watford 2-0 West Ham

West Brom 2-3 Leicester

19:55 Mechi zinamalizika

19:47 Man City wanapata penalti nyingine lakini Aleksandar Kolarov anashindwa kufunga.

19:46 Man City 2-1 Norwich City

Man City warejea kileleni mwa Ligi ya Premia baada ya Yaya Toure kufunga penalti.

19:44 Man City wanapewa penalti.

Kadi nyekundu

19:42 Watford 2-0 West Ham

James Collins wa West Ham anapewa kadi nyekundu.

19:42 West Brom 2-3 Leicester

Rickie Lambert afunga penalti dakika ya 84. West Brom sasa wamepungukiwa na bao moja kulipa deni.

19:42 Manchester City 1-1 Norwich

Cameron Jerome asawazishia Norwich.

19:35 BAOOO! West Brom 1-3 Leicester

Jamie Vardy aongezea Leicester la tatu.

Jamie sasa amefunga bao katika mechi nane mfululizo ligini. Ni Daniel Sturridge (9) na Ruud van Nistelrooy (10) pekee waliomzidi.

19:31 BAOOOOO! Swansea 0-3 Arsenal

Joel Campell afungia Arsenal bao la tatu dakika ya 72. Bila shaka sasa alama tatu ziko mkobani.

19:30 Manchester United wataka wapewe penalti baada ya Ander Herrera kuanguka baada ya kukabiliwa na Damien Delaney. Wananyimwa.

19:29 Gomis achomoka upande wa Swansea na kulenga goli la Arsenal. Lakini amejenga kibanda ardhi ya wenyewe.

19:26 Swansea 0-2 Arsenal

Laurent Koscielny afungia Arsenal dakika ya 68.

19:23 BAOOOO! Manchester City 1-0 Norwich

Nicolas Otamendi afungia City baodakika ya 68.

19:20 BAOOOO! West Brom 1-2 Leicester

Riyad Mahrez aongezea Leicester bao la pili.

19:18 Arsenal wanafanya kaunta. Lakini Ozil ameotea.

19:18 Campel anatoa krosi safi na Giroud anaikimbilia. Lakini kipa wa Swansea anaufikia mpira kabla yake.

19:17 BAOOOO!

West Brom 1-1 Leicester

Riyad Mahrez anasawazishia Leicester.

19:12 Swansea 0-1 Arsenal

Ayew ambwaga kipa Cech. Wachezaji wa Arsenal wanazuia mpira kuingia. Lakini halingehesabiwa, alikuwa kaotea.

19:06 BAOOOO! Swansea 0-1 Arsenal

Olivier Giroud aweka Arsenal kifua mbele kwa kufungwa kwa kichwa baada ya kona kupigwa na Alexis Sanchez. Hilo ni bao la 2,000 kwa Arsenal chini ya Wenger.

19:05 Crystal Palace 0-0 Man Utd

Chris Smalling apewa kadi ya njano kwa kumuangusha Dwight Gayle.

18:03 BAOOO Watford 2-0 West Ham

Odion Ighalo afungia Watford.

Mechi zinaanza tena.

Ni wakati wa mapumziko sasa

Crystal Palace 0-0 Man Utd

Man City 0-0 Norwich

Newcastle 0-0 Stoke

Swansea 0-0 Arsenal

Watford 1-0 West Ham

West Brom 1-0 Leicester

18:44 Swansea 0-0 Arsenal

Giroud amelala chini na anaonekana kuumia baada ya kugongwa mguuni na Montero. Baada ya kuhudumiwa kwa muda ndani ya uwanja, anatoka nje.

18:38 BAOOO! Watford 1-0 West Ham

Aaron Cresswell anajifunga.

18:34 Kipa John Ruddy anafanya kazi ya ziada kuzuia Manchester City kujiweka kifua mbele Etihad. Anazima frikiki ya Yaya Toure kutoka hatua 20 ndani ya uwanja.

18:29 BAOOO!West Brom 1-0 Leicester

Salomon Rondon (Dakika ya 30)

Rondon anamponyoka Danny Simpson na kufunga bao kwa kichwa.

18:28 Swansea 0-0 Arsenal

Baada ya kushambuliwa kwa muda, wakihangaishwa na Bafetimbi Gomis, Arsenal wanapata nafasi. Lakini Olivier Giroud anatuma mpira wake juu ya goli.

18:24 Crystal Palace 0-0 Man Utd

Wayne Rooney anapata frikiki hatua 25 kutoka kwenye goli. Mpira wake unaenda moja kwa moja hadi mikononi mwa kipa.

18:22 Manchester City 0-0 Norwich

Wilfried Bony anapata nafasi wazi akibaki na kipa John Ruddy pekee, kombora lake analituma nje.

18:16 Swansea 0-0 Arsenal

Joel Campbell anakaribia kufunga lakini wapi, mpira wake unakosa goli pembamba.

Baadaye Mourinho amekubali kuzungumza na wanahabari na kusema wachezaji wake wanajitolea kabisa lakini kuna mambo yaliyotokea wakati wa mechi na kubadilisha mambo. Amesema bado hana wasiwasi kuhusu kazi yake.

18:15 Manchester City 0-0 Norwich

Norwich wanatawala Etihad kwa sasa.

18:11 Crystal Palace 0-0 Man Utd

Mpira unagonga mwamba! Kombora la Yannick Bolasie linagonga mwamba wa goli na kutoka nje. Vijana wa Alan Pardew wanaonekana kudhibiti mpira kwa sasa. Mpira wa kichwa wa Scott Dann unatupwa juu ya goli na David De Gea.

18:08 Swansea 0-0 Arsenal

Arsenal wanapata nafasi. Kwa bahati mbaya, mpira unamwangukia Nacho Monreal, kombora lake kutoka kwa krosi ya Joel Campbell linatoka nje.

Mourinho baada ya kuulizwa maswali na wanahabari kuhusu matokeo ya leo, amewajibu: "Sina la kusema."

Kwingineko, timu zimetangazwa: Mechi hizi 18:00 saa za Afrika Mashariki.

Cyristal Palace v Manchester United

Manchester United XI: De Gea, Darmian, Blind, Smalling, Rojo, Schneiderlin, Schweinsteiger, Herrera, Mata, Martial, Rooney.

Crystal Palace XI: Hennessey, Kelly, Dann, Delaney, Ward, McArthur, Cabaye, Zaha, Puncheon, Bolasie, Gayle.

Man City v Norwich City

Man City XI: Hart, Sagna, Kompany, Otamendi, Kolarov, Toure, Fernandinho, Navas, De Bruyne, Bony, Iheanacho

Norwich City XI: Ruddy, Bennett, Martin, Bassong, Brady, Mulumbu, Tettey, Olsson, Howson, Jarvis, Jerome

Swansea v Arsenal

Swansea City XI: Fabianski, Naughton, Fernandez, Williams, Taylor, Ki Sung-Yueng, Shelvey, Ayew, Sigurdsson, Montero, Gomis.

Arsenal XI: Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ozil, Campbell, Sanchez, Giroud.

Mechi yamalizika Chelsea 1-3 Liverpool

Dakika ya 90+4: Mechi inamalizika. Mourinho anamsalimia Klopp na kuondoka uwanjani.

Dakika ya 90+2: Zouma anatuma krosi eneo la hatari lakini inapaa juu na kutoka nje.

Dakika ya 90+1: Adam Lallana anaondolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Dejan Lovren

Dakika ya 90: Coutinho anashambulia tena. Anapata kona. Mpira unarejeshwa safu ya kati na kisha kwa kipa wa Liverpool.

Haki miliki ya picha AP

Dakika ya 82: BAOOOO! Christian Benteke!Chelsea 1-3 Liverpool.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Utafutwa asubuhi" mashabiki wanaimba wakimkejeli Mourinho. Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wanaanza kuondoka uwanjani. Wengine bado wanaimba jina lake.

Dakika ya 80: Chelsea wanashambuliwa tena. Nusura bao liingie.

Dakika ya 75: Alberto Moreno anapata nafasi na kushambulia. Kipa wa Chelsea Begovic anachomoka na kutupa nje kombora lake.

Dakika ya 73: BAOOOOOO! Coutinho! Chelsea 1-2 Liverpool.

Dakika ya 71: Cesc Fabregas anaingizwa nafasi ya John Obi Mikel, huku Chelsea wakiendelea kushambulia.

Dakika ya 70: Chelsea wanapata kona. Inachapwa na Willian lakini haizai matunda.

Dakika ya 68: Lucas Leiva ambaye tayari ana kadi ya njano anamchezea vibaya Ramires. Wachezaji wa Chelsea wanamzingira Mark Clattenburg. Lakini refa hachukui hatua yoyote. Anamuonya tu mchezaji huyo.

Dakika ya 63: Emre Can anapewa kadi ya njano.

Dakika ya 62: Nahodha wa Liverpool James Milner anaondolewa uwanjani na utepe wa unahodha unakabidhiwa Martin Skrtel.

Dakika ya 61: Kenedy nusura afanye mambo. Kenedy anatoa kombora kutoka hatua 18 lakini linaenda nje.

Ramires naye anapata nafasi nzuri lakini mpira wake unazuiwa na Martin Skrtel na Emre Can.

Dakika ya 59: Eden Hazard anatolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Mbrazil Kenedy.

Dakika ya 57: Lucas anaonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 49: Liverpool wanashambulia. Cahill anautoa mpira nje kwa kichwa na inakuwa kona. Tena Cahill anautoa nje wakati huu kwa mguu. Kona nyingine inapigwa lakini kombora la Coutinho linapaa na kupitia juu ya goli.

Dakika ya 49: Ramires anatoka nyuma na kumkabili Coutinho safu ya kati. Refa anatoa frikiki.

Dakika ya 47: Liverpool wanapata nafasi nzuri. Firmino ana mpira, lakini Zouma anaufikia na kuupiga nje.

Dakika ya 46: Chelsea wanashambulia. Lakini kombora la Willian linapinduliwa kisha kunyakwa na kipa.

Mechi inaanza kipindi cha pili.

Ni muda wa mapumziko sasa. Chelsea 1-1 Liverpool

Dakika ya 45+3: BAOOOO! Coutinho anasawazishia Liverpool. Chelsea 1- 1 Liverpool

Haki miliki ya picha Reuters

Dakika ya 41: Diego Costa anakimbiza mpira eneo la Liverpool lakini unatoka nje kabla yake kuufikia.

Dakika ya 37: Mpira wa mbali unatumwa eneo la hatari la Chelsea. Lucas anaufikia kwa kichwa lakini mpira wake unanyakwa na kipa. Zouma analala chini akionekana kuumia lakini baadaye anainuka na kuendelea na mechi.

Dakika ya 35: Liverpool wanadai Terry amenawa mpira baada ya kutuliza krosi ya Nathaniel Clyne kwa kifua. Refa anakataa.

Dakika ya 32: Lucas crashes anagongana na John Obi Mikel. Anataka apewe frikiki lakini refa anakataa.

Dakika ya 29: Emre Can anaponyoka kadi ya njano kwa kumwangusha Willian karibu na eneo la kuchapiwa kona. Anaonywa na refa.

Dakika ya 26: Roberto Firminio anatuliza mpira upande wa Liverpool, anatuma mpira mzuri unaomfikia James Milner na kwa pamoja na Nathaniel Clyne wanapanga shambulio kali. Milner anatuma krosi kurua lakini mpira wa Lallana unatua mikononi mwa Begovic

Dakika ya 24: Willian anatamba kwenye wingi. Anafyekwa na Coutinho ambaye analishwa kadi ya njano.

Dakika ya 22: Liverpool wanapata kona nyingine baada ya Terry kuutoa nje mpira. Kona inapigwa na kudakwa na kipa Begovic.

Dakika ya 15: Liverpool wameanza kutulia na wanaonekana kuwa hatari. Wanapata kona lakini mpira wa Philippe Coutinho unatua mikononi mwa kipa Asmir Begovic.

Dakika ya 14: Nathaniel Clyne anapata nafasi tena. Anatoa kombora lakini linatoka nje.

Dakika ya 11: Nathaniel Clyne anashambulia kutoka wingi ya kulia, anamkabili Cesar Azpilicueta na kisha kutoa krosia ambayo inadakwa na kipa wa Chelsea Asmir Begovic.

Dakika ya 10: Liverpool wanashambulia ngome ya Chelsea wakiongozwa na Coutinho.

Dakika ya 9: Mamadou Sakho analazimika kutumia kichwa kuondoa mpira eneo la hatari.

Dakika ya 6: Mashabiki wameanza kuimba jina la Mourinho: "Jose Mourinho, Jose Mourinho...."

Dakika ya 5: Chelsea wanakaribia sana kufunga. Lakini Liverpool wanaondoa mpira eneo la hatari.

Dakika ya 4: BAOOOO! Chelsea 1-0 Liverpool

Ramires anafunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi kutoka kwa Cesar Azpilicueta.

Image caption Ramires anapongezwa na wachezaji wenzake

15: 45: Mpira unaanza.

15:40 Wachezaji wa timu zote mbili wanaingia uwanjani sasa. Mechi inaanza 15:45. Kumbuka ni kivumbi kati ya Mourinho na Klopp.

Haki miliki ya picha Getty

15:15: Timu zimetangazwa

Liverpool XI: Mignolet, Clyne, Skrtel, Sakho, Moreno, Lucas, Can, Milner, Lallana, Coutinho, Firmino.

Chelsea XI: Begovic; Zouma, Cahill, Terry (c), Azpilicueta; Mikel, Ramires; Willian, Oscar, Hazard; Diego Costa.

15:10: Chelsea leo wako nyumbani dhidi ya Liverpool katika Ligi ya Premia kwenye mechi ya mapema ambayo wengi wanaamini huenda ikaamua hatima ya Meneja wa Chelsea Jose Mourinho.

Chelsea imeandikisha matokeo mabaya sana na itakuwa vigumu sana kwao kutetea taji la ligi ambalo walishinda msimu uliopita.

Meneja wao amesema hana uhakika pia kuhusu iwapo wataweza kumaliza katika nne bora na kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Hata hivyo amesema hana wasiwasi kuhusu kazi yake.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Liverpool, ambao wana meneja mpya Mjerumani Jurgen Klopp, wameshinda mechi tatu mfululizo Stamford Bridge mwaka 2011 lakini hawajashinda hata mechi moja tangu wakati huo.

Klopp amesema anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Chelsea hata ingawa mambo hayawaendei sawa msimu huu.

Haki miliki ya picha Reuters

Mechi nyingine zinazochezwa leo (Saa za GMT)

Crystal Palace v Man Utd 15:00

Man City v Norwich 15:00

Newcastle v Stoke 15:00

Swansea v Arsenal 15:00

Watford v West Ham 15:00

West Brom v Leicester 15:00