Aston Villa hoi yapigwa na Tottenham 3-1

Haki miliki ya picha PA
Image caption Aston Villa na Tottenham wakimenyana

Boss mpya wa Aston Villa Remi Garde amepokelewa kwa kipigo kutoka kwa Tottenham katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia jumanne.

Kabla hata hajakaa vizuri kwenye kitu ndani ya dakika tatu za kwanza za mchezo Aston Villa ilikuwa tayari imepigwa bao la kwanza. Baadaye likafuata jingine dakika ya 45.

Ingawa Aston Villa ilijaribu kufurukuta kwa kupata bao dakika ya 79 lakini wakazidiwa nguvu dakika ya 90. Hadi mwisho wa mpira Tottenham ikawa imeiadhibu Aston Villa 3 -1