Mourinho akana kuwepo kwa mgomo Chelsea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mourinho

Mkufunzi wa kilabu ya chelsea Jose Mourinho amekana madai kwamba kuna mgomo baridi miongoni mwa wachezaji katika kilabu ya Chelsea.

Mapema siku ya jumanne,kiungo wa kati wa kilabu hiyo Cesc Fabregas alikana ripoti kwamba alikuwa anapanga mgomo mdogo katika kilabu hiyo.

Chelsea iko nafasi ya 15 katika jedwali la ligi ya Uingereza,baada ya kupoteza mechi sita kati ya mechi 11 msimu huu.

''Ni shutuma mbaya sana ,kwa kuwa unawatuhumu wachezaji ama mchezaji kwa kutokuwa waaminifu''.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Fabrigas

Alipoulizwa iwapo ni kweli kwamba mchezaji muhimu sana katika timu hiyo alisema kwamba ''yuko tayari kupoteza mechi badala ya kumshindia ''Mourinho'' kama ilivyoripotiwa na BBC 5 Radio,nahodha wa kilabu hiyo John Terry amesema kuwa katika maisha yake yote hajasikia mchezaji akitamka maneno kama hayo.