Mourinho apewa adhabu kukosa mechi moja

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jose Mourinho mwenye koti jeusi

Shirikisho la soka barani Ulaya, limempa adhabu Meneja wa Chelsea Mourinho ya kuikosa mechi moja na kutakiwa kulipa faini ya pauni elfu 40 za uingereza.

Kosa hilo linakuja kutokana na Mourinho kukiri kosa la kutumia lugha isiyokubalika walipopigwa na West Ham tarehe 24 mwezi uliopita.

Sasa ataikosa mechi ya Ligi jumamosi labda labda akikata rufaa.

Wiki hii atakabishiwa barua ya sababu za adhabu yake lakini kama atajitetea na kuwashawishi pengine tutamwona kwenye benchi akiipigania nafasi yake.

Adhabu hii ya kutimuliwa uwanjani haihusiani na ile ambayo alipigwa kutokana na maneno yake ya tarehe 3 mwezi uliopita na pia kutakiwa kulipa pauni elfu 50 walipopigwa na Southampton.