Afrika yajihakikishia ubingwa kombe la vijana

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nigeria imeshinda kombe hilo mara nne

Afrika imejihakikishia ubingwa wa Kombe la Dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17 baada ya mataifa mawili ya Afrika kufika fainali.

Fainali hiyo itachezwa Jumapili kati ya Nigeria, ambao ndio mabingwa watetezi, na Mali nchini Chile.

Nigeria wameshinda dimba hilo mara nne; 1985, 1993, 2007 na 2013.

Nigeria walifika fainali kwa kuulaza Mexico 4-2 nao Mali kwa kucharaza Ubelgiji 3-1 kwenye nusu fainali.

Orji Okwonkwo alikuwa miongoni mwa waliofungia mabao Nigeria

Haki miliki ya picha Other

Osinachi Ebere, Kelechi Nwakali na Victor Osimhen walifungia Golden Eaglets mabao hayo mengine. Nigeria, ambao ndio mabingwa watetezi, wanaongoza kwa kushinda kombe hilo mara nyingi, wakifuatwa na Brazil walioshinda kombe hilo mara tatu (1997, 1999 na 2003). Ghana wanafuata kwa kutwaa ubingwa mara mbili (1991 na 1995).

Sidiki Maiga alifungia Mali bao lao la pili na kuwasaidia kuchapa Ubelgiji.

Haki miliki ya picha AFP

Boubacar Traore na Sekou Koita walifungia Mali mabao hayo mengine.

Haki miliki ya picha AFP