Nigeria mabingwa wa dunia

Nigeria
Image caption Nigeria walikuwa ndio mabingwa watetezi

Timu ya taifa ya vijana ya Nigeria Golden Eaglets chini ya miaka 17 imetwaa ubingwa wa kombe la dunia kwa vijana.

Nigeria iliwachapa Mali katika mchezo wa fainali kwa mabao 2-0. Mshambuliaji Victor Osimhen ndiye aliyeanza kuipatia timu yake bao la kwanza na Funsho Ibrahim Bamgboye akaongeza bao la pili na la ushindi.

Kikosi cha cha vijana cha Nigeria kimeweza kutetea ubingwa wake baada ya kutwaa taji hilo la dunia la vijana mwaka 2013 walipoishinda Mexico kwa mabao 3-0.

Mshambuliaji Victor Osimhen ameibuka mfungaji bora kwa kuzipasia nyavu jumla ya mabao 10 katika michuano hiyo.

Afrika ilikuwa tayari imejihakikishia ubingwa wa dunia baada ya mataifa hayo mawili, Nigeria na Mali kufika fainali.