Rais wa chama cha soka Ujerumani ajiuzulu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wolfgang Niersbach

Rais wa Chama cha Soka Ujerumani DFB Wolfgang Niersbach amejiuzulu kwa tuhuma za ukwepaji kodi na kujihusisha na rushwa.

Inadaiwa maafisa wa shirikisho la soka duniani walipewa hongo wakati wa mchakato wa kuipa Ujerumani zabuni ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia 2006.

Novemba 3, polisi wa Frankfurt walivamia makao makuu ya chama cha soka Ujerumani kwa uchunguzi wa madai ya ukwepaji kodi katika chama hicho kuhusiana maandilizi ya kombe la dunia.

Chama cha soka cha Ujerumani kilikana madai hayo mwezi uliopita na Wolfgang Niersbach amesema: "Mimi nilihusika katika jitihada kwa ajili ya Kombe la Dunia 2006 kuanzia siku ya kwanza mpaka nyaraka za mwisho za majira zilizowezekana ziliwasilishwa."

Niersbach alisema."Napenda kuweka wazi bila shaka kwa mara nyingine tena kwamba kulikua hakuna habari kwamba kulitolewa pesa zozote."

Pia kiongozi huya amesema yeye alichukua wajibu wa kisiasa kwa malipo yaliyotolewa kwa Fifa ya thamani ya Euro 6.7m (£ 4.9M) Nyumba za Niersbach, mtangulizi wake Theo Zwanziger, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Horst Schmid, zilifanyiwa uchunguzi