Timu ya Algeria kuwasili Tanzania

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Timu ya taifa ya Algeria

Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria unatarajiwa kuwasili Tanzania kesho kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65.

Msafara huo utajumuisha wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha mkuu wa timu hiyo Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.

Mchezo huu wa raundi ya pili ni wa kuwania kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la dunia litakalofanyika huko nchi Urusi mwaka 2018.