Kenya yaichapa Cape Verde, Rwanda yalazwa

Stars
Image caption Mechi ya marudiano itachezwa Jumanne nchini Cape Verde

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeondoka na ushindi dhidi ya Cape Verde mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia iliyochezewa Nairobi.

Kenya imeilaza Cape Verde 1-0 kwenye mechi hiyo ya raundi ya pili ya kufuzu kwa fainali zitakazochezewa Urusi mwaka 2018.

Bao pekee la Harambee Stars limefungwa na Michael Olunga anayechezea klabu ya Gor Mahia dakika ya tisa.

Mechi ya marudiano itachezewa mjini Praia Jumanne ijayo.

Kwingineko, Rwanda hawakuwa na bahati kwani wamelazwa 1-0 na Libya kwenye mechi iliyochezewa nchini Tunisia kutokana na ukosefu wa usalama Libya.

Faisal Al Badri alifunga bao hilo muda mfupi baada ya mapumziko.

Mechi ya marudiano itachezewa Kigali Jumanne ijayo.

Matokeo ya mechi zote za leo ni kama ifuatavyo:

  • Madagascar 2-2 Senegal
  • Comoros 0-0 Ghana
  • Kenya 1-0 Cape Verde
  • Libya 1-0 Rwanda
  • Angola 1-3 Afrika Kusini
  • Niger 0-3 Cameroon
  • Liberia 0-1 Ivory Coast

Taifa Stars ya Tanzania itashuka dimbani kesho saa kumi unusu alasiri kuchuana na Algeria.