Mvua yaahirisha mchezo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha wa Argentina

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Brazil na Argentina umeahirishwa sababu ya mvua nyingi kunyesha.

Mchezo huo iliokua uchezwe usiku wa siku ya alhamisi katika uwanja wa Estadio Antonio Vespucio Libert, mjini Buenos Aires sasa utachezwa usiku wa siku ya ijumaa.

Sehemu ya kuchezea ya uwanja huo ulijaa maji na washabiki wa soka pamoja na maafisa wa timu ya Brazil walikwama njiani kwenye foleni sababu ya mvua kubwa iliyonyesha.

Kocha msaidizi wa Brazil Gilmar Rinaldi, alisema "tulikutana na maafisa wa soka wa Argentina tukazungumza na hakukua na namna ya mchezo kuchezwa.

Katika mchezo huu Argentina itamkosa Nahodha wake Lionel Messi anayesumbuliwa na maumivu wakati Brazil itakuwa nae tena Nahodha wao Neymar Jr ambae hakucheza Mechi 2 za mwanzo akutokana na kuwa adhabu ya kutocheza michezo minne.