Nani mwanasoka bora wa Afrika 2015?

Hawa ndio wachezaji watano wanaowania tuzo ya BBC ya Mwanakandanda bora wa Afrika wa mwaka huu 2015.

Wachezaji hao ni:

1. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon na Borussia Dortmund (Ujerumani)

2. André Ayew - Ghana na Swansea City (Uingereza)

3. Yacine Brahimi - Algeria na FC Porto (Ureno)

4. Sadio Mané - Senegal na Southampton (Uingereza)

5. Yaya Touré - Ivory Coast na Manchester City (Uingereza)

Asante sana kwa wale waliopiga kura.

Kwa sasa upigaji kura umefungwa.

Mshindi atatangazwa tarehe 11 mwezi Desemba.

Walioshinda Tuzo ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka kwa miaka iliyotangulia ni:

Yacine Brahimi (2014);

Yaya Touré (2013);

Christopher Katongo (2012);

André Ayew (2011);

Asamoah Gyan (2010).