Mechi ya Uingereza dhidi ya Ufaransa kuchezwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wa timu ya Ufaransa

Mechi ya kirafiki kati ya Uingereza na Ufaransa katika uwanja wa Wembley itaendelea kama ilivyopangwa siku ya jumanne baada ya msururu wa mashambulio ambayo yamewaua takriban watu 128.

Washambuliaji 3 wa kujitolea muhanga walifariki katika milipuko nje ya uwanja wa stade de France huku wachezaji wa Ufaransa wakicheza dhidi ya Ujerumani siku ya ijumaa.

Lakini rais wa shirikisho la soka la Ufaransa FFF Noel le Gaet amesema kuwa Les Blues itasafiri mjini Landon.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mchezaji wa Uingereza Wayne Rooney

Shirikisho la soka nchini Ufaransa limesema kuwa :kwa pamoja na shirikisho la soka la Ufaransa FFF tunaunga mkono uamuzi huo.

FA pia imesema kuwa mechi ya Uingereza itakayowashirikisha vijana walio chini wa umri wa miaka 20 dhidi ya Ufaransa siku ya jumamosi imeahirishwa.