Afisa wa riadha Kenya anachunguzwa na IAAF

Image caption David Okeyo

Mwanakamati wa shirikisho la riadha duniani IAAF David Okeyo anachunguzwa na maafisa wa kupambana na ufisadi nchini Kenya na kamati ya uadilifu ya shirikisho la riadha duniani IAAF kuhusu ''kutoweka kwa fedha za udhamini wa kampuni inayoipa timu ya taifa ya riadha mavazi Nike''.

Okeyo ambaye mwenyewe ni naibu wa rais wa shirikisho la riadha la Kenya AK, anatuhumiwa kwa 'kufyonza pesa zilizolipwa kwa shirikisho la riadha kama malipo ya ufadhili wa kampuni ya kutengeneza bidhaa za michezo Nike.'

Amekanusha madai yote dhidi yake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption IAAF imewapiga marufuku wanaridha wa Urusi kutoshiriki mashindano yeyote

Habari hizi bila shaka ni msumari wa moto juu ya kidonda kwa shirikisho la riadha dunini IAAF ambayo majuzi tu iligonga vichwa vya habari kote duniani, baada ya aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Lamine Diack, kupatikana na hatia ya kupokea hongo kutoka kwa Urusi.

Yamkini Diack alikuwa akizuia uchunguzi dhidi ya wanariadha wa Urusi walioshukiwa kuwa walikuwa wametumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini

IAAF imeipiga marufuku Urusi kutoka kwenye mashindano ya riadha kufuatia ripoti ya shirika linalopigana dhidi ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini WADA kuipata shirikisho la riadha nchini humo na hatia ya utepetevu wa kutekeleza masharti makali ya kupambana dhidi ya utumizi wa dawa hizo haramu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa rais wa shirikisho la riadha IAAF Lamine Diack, anakabiliwa na shtaka la kupokea hongo kutoka kwa Urusi.

Kupitia kwa taarifa ya shirikisho la riadha duniani " IAAF haijafahamishwa kuhusu madai na tuhuma dhidi ya mwanakamati wake David Okeyo hata hivyo habari za matukio ya liosababishwa achunguzwe sasa imekabidhiwa kamati ya nidhamu na maadili iliuchunguzi wa kina ufanywe''.

Msemaji wa kampuni hiyo ya kutengeza bidhaa za michezo kutoka Marekani Nike ameiambia gazeti la Sunday Times kuwa kampuni hiyo ''ilishirikiana kwa uadilifu na uwazi na shirikisho la riadha la Kenya na kuwa hakuna dosari yeyote iliyotokea kwani fedha walizotoa zilinuiwa kuwezesha timu ya taifa ya riadha ya Kenya ''

Aliongezea kusema kuwa Nike inashirikiana na maafisa wa upelelezi nchini Kenya.