Lambert kocha mpya Blackburn Rovers

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Paul Lambert,kocha mpya wa Blackburn Rovers

Kocha wa zamani wa Aston Villa Paul Lambert ameteuliwa kocha mpya wa klabu ya Blackburn Rovers baada ya Gary Bowyer kufutwa kazi.

Lambert mwenye umri wa miaka 46 alifukuzwa na klabu hiyo ya Aston Villa mwezi Februari ambapo anasema kuwa kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa nje ya timu hiyo anajiona aliyeimarika zaidi na kwamba kwa sasa anaangalia mbele. Bowyer alitimuliwa kutokana na kufanya vibaya kwa klabu biyo. Kati ya mechi 10 za ligi walizocheza alishinda mbili tu na kuifanya klabu yake ya Rovers kushika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi.