Je, Sterling alifanya uamuzi mzuri kuondoka Liverpool?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling

Watu wengi wanasema kuwa Raheem Sterling hakufanya uamuzi wa busara alipojiunga na kilabu ya Manchester City kutoka liverpool kwa kitita cha pauni milioni 49.

Kulikuwa na maswali mengi kuhusu mda atakaopewa kucheza ,kwa kuwa ni wachezaji wawili walio chini ya umri wa miaka 21 ambao wamecheza mechi nyingi za ligi ya Uingereza kumshinda.

Kulingana na aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Ian Wright Sterling hachezi tu bali anacheza vizuri.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raheem Sterling

Wright anasema kuwa ijapokuwa hajaleta mchango mkubwa anapochezea City ikilinganishwa na wachezaji wengine kama vile Kevin De Bryune,kulingana na mabao na usaidizi, lakini ameanza vyema.

Ameongezea kuwa kitu ambacho kitaiathiri tamaa ya Raheem ni kwamba ametolewa kabla ya mechi kuisha katika mechi 10 alizoanza kufikia sasa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raheem Sterling alipokuwa akiichezea Liverpool
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raheem Sterling alipokuwa akiichezea Liverpool

Lakini hilo linafaa kumpatia motisha kwamba bado ni kijana mdogo ambaye anafaa kurekebisha udhaifu wake pamoja na uwezo wakeraheem Sterling alipokuwa akiichezea LiverpoolAna miaka 20 pekee na mengi yanatarajiwa kutoka kwake.

Ana uwezo kuwa mmoja wa wachezaji mahiri lakini hilo hawezi kuliafikia bila jitihada.