El Classico:Je, Messi na Benzema watacheza?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Messi na Ronaldo

Mkufunzi wa kilabu ya Barcelona Louis Enrique ataamua saa moja kabla ya mchuano wa El Classico iwapo nyota wa timu hiyo Lionel Messi atacheza dhidi ya Real Madrid au la baada ya kupona jereha.

Real Madrid ambayo itaipiku Barcelona katika kilele cha ligi hiyo iwapo itashinda ina kikosi kamili.

''Tunajua kwamba hatokuwa asilimia 100.Iwapo atacheza au la,habari njema ni kwamba amepona jeraha'',alisema Enrique.Sijapanga lolote.Nitazungumza na leo siku ya Jumamosi .Saa moja kabla ya mechi hiyo ya kukata na shoka tutaamua''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Barcelona

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema,ambaye anachunguzwa kwa kuhusishwa na usaliti wa kanda ya ngono na ambaye anasema kuwa hakuhusika katika kashfa hiyo amekosa mechi sita kutokana na jeraha.

''Benzema yupo katika kikosi,alifanya mazoezi vizuri na ni miongoni mwa kikosi changu'',Meneja wa Real Madrid Rafael Benitez alisema.''Bado tunajadiliana iwapo ataanzishwa au la''.