Rwanda ni mabingwa wa 'Tour of Rwanda'

Image caption Jean Bosco Nsengimana mwenye umri wa miaka 22 ameibuka mshindi wa mashindano ya Tour of Rwanda

Timu ya waendeshaji baiskeli kutoka Rwanda ilinawiri katika mashindano ya kimataifa ya Tour of Rwanda yaliyomalizika mjini Kigali.

Timu ya Rwanda ilihifadhi ubingwa wa mashindano hayo Tour of Rwanda.

Jean Bosco Nsengimana mwenye umri wa miaka 22 ameibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyozunguka Rwanda kwa wiki nzima yakishirikisha jumla ya waendesha baiskeli 60 kutoka kona zote duniani.

Nsengimana aliwashinda nguvu wenzie wa timu ya Rwanda Joseph Aleluya aliyemaliza katika nafasi ya pili na Camera Hakuzimana aliyechukua nafasi ya tatu.

Image caption Kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa timu kutoka Eritrea.

Kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa timu kutoka Eritrea.

Pia gwiji wa mchezo huo Debesay Mekseb ,mwenye uraia wa Eritrea lakini akichezea timu ya Bike Aid ya Ujerumani , licha ya kushinda awamu 4 kati ya awamu 7 za mashindano hayo hakuweza kupangua dakika 3 ambazo wanyarwanda walimzidi.

Hii ni mara ya pili mfululizo waendesha baiskeli hao kutoka Rwanda kunyakua taji kuu katika mashindano hayo ya Tour of Rwanda yaliyoko kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za baiskeli barani Afrika yanayotambuliwa na shirikisho la dunia la mbio za baiskeli.