Tottenham yatakata Ligi Kuu England.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mpambano kati ya Tottenham na West Ham

Klabu ya soka ya Tottenham Hotspur jana ilifanikiwa kuvuna ushindi mnono na kukwea hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi.

Baada ya kuitandika West Ham 4-1 kwa mchezo pekee uliopigwa Jumapili katika uwanja wa White Hart Lane.

Mabao ya Spurs yalifungwa na wachezaji Harry Kane, Toby Alder-weireld na Kyle Walker.

Bao la kufutia machozi la West Ham lilifungwa na Manuel Lanzin.