Sunderland yaipiga Crystal Palace

Image caption Crystal Palace

Klabu ya soka ya Sunderland imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wakiwa ugenini baada ya kuifunga Crystal Palace 1-0.

Bao pekee la ushindi la Sunderland lilifungwa na Jermain Defoe.

Ushindi huo umewaweka Sunderland katika nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 9 baada ya kucheza mechi 13.

Ligi ya England inatarajia kuendelea tena Jumamosi ya Novemba 28 kwa michezo mbalimbali ambapo, Aston Villa watakuwa wenyeji wa Watford.

Bournemouth watawaalika Everton, Crystal Palace watawakaribisha Newcastle, Man City watakuwa wenyeji wa Southampton, Sunderland wataumana na Stoke huku Leicester city wakiwakaribisha Man United.