Kilimanjaro Stars yachanja mbuga Cecafa

Kenya
Image caption Kenya leo itachuana na Burundi

Michuano ya Cecafa iliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi, Kilimanjaro Stars wakiandikisha ushindi mwingine.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya robo fainali.

Mabao ya Kilimanjaro stars yalifungwa na Said Ndemla pamoja na Simon Msuva huku bao la Rwanda likifungwa na mchezaji Tisiyege.

Zanzibar hata hivyo walifungwa 4-0 na Uganda ikiwa ni mechi ya Kundi B.

Michuano hiyo itaendelea tena leo Jumatano kwa mechi kadhaa ambapo Kenya itachuana na Burundi.

Somalia itaivaa Ethiopia, Malawi itaikabili Djibouti na Sudan kusini watachuana na ndugu zao Sudan.