Tyson Fury 'atarambishwa sakafu'

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wladmir Klitschko

Wladimir Klitschko atamuangusha Tyson Fury wakati wawili hao watakapopigana katika mji wa Dusseldorf siku ya jumamosi kulingana na bondia wa uzani mzito nchini Uingereza Anthony Joshua.

Klitschko mwenye umri wa miaka 39 amekuwa bingwa wa dunia katika uzani huo tangu mwaka 2006,akiwa amepigana mapigano 27 na kufanikiwa kuyatetea mataji yake mara 23.

Atakuwa akitetea taji lake la WBA ,IBF na WBO dhidi ya raia wa Uingereza Tyson Fury.

''Itakuwa vyema iwapo Fury atashindfa ,lakini namuunga mkono Klitschko katika raundi ya tano au sita'',Joshua aliiambia BBCsport.

Image caption Wawili hawa watazipiga siku ya jumamosi

''Fury atajitokeza na kupigana ,hasira zitamdanganya na kuuonyesha mwili wake.Yeye hurusha makonde mengi na hutembea sana ikilinganishwa na mtu mwenye uzani mkubwa kama wake lakini Klitschko ana uzoefu mwingi ,amekuwa akitetea taji lake kwa miaka 10''.