Van Gaal:Tutashinda Wolfsburg

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amekiri kwamba klabu hiyo inakabiliwa na mechi ngumu itakapokutana na Worlfsburg katika mechi ya mwisho ya mechi ya kufuzu katika mkondo wa muondoano wa kombe la vilabu bingwa Ulaya.

United iko pointi moja nyuma ya viongozi wa kundi hilo Wolfsburg kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya PSV Eindhoven.

Timu hiyo sasa inahitaji ushindi ili kufuzu kwa kuwa iko pointi moja juu ya PSV ambao wana mabao mengi.

''Lolote lawezekana, tunaweza kushinda mahala popote'', alisema Van Gaal.Tumedhihirisha hilo katika ligi ya Uingereza na lazima tufanye hivyo katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya''.

''Tumejiwekea vigingi kabla ya mechi hiyo ya mwisho lakini tutaenda Ujerumani tukiwa na matumaini''.