Dibaba atawazwa mwanariadha bora wa mwaka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dibaba alishinda mbio za 1500m jijini Beijing

Mwanariadha kutoka Ethiopia Genzebe Dibaba ameshinda tuzo ya Mwanariadha Bora wa Mwaka inayotolewa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) upande wa wanawake.

Ameshinda tuzo hiyo baada ya kuvunja rekodi za dunia katika mbio za 1500m nje ya ukumbi, 5000m ndani ya ukumbi na kwa kutwaa dhahabu 1500m katika mashindano ya ubingwa wa riadha duniani mjini Beijing.

Baada ya kushinda tuzo hiyo, amesema anapanga kuvunja rekodi ya kukimbia maili moja kwenye ukumbi.

Anatoka kwenye familia yenye wanariadha wengi. Ndugu zake wawili na binamu mmoja wameshinda dhahabu michezo ya Olimpiki.

Tuzo ya wanaume imemwendea Ashton Eaton wa Marekani.