Daniel Sturridge apata jeraha jingine

Haki miliki ya picha PA
Image caption Danniel Sturridge kushoto

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amepata jereha jingine la mguu wakati wa mazoezi ambalo lilimuweka nje katika mechi dhidi ya Bordeaux katika ligi ya Yuropa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alitarajiwa kurudi siku ya Alhamisi baada ya kuuguza jereha ambalo lilimuweka nje tangu mwezi Octoba.

Hatahivyo,mchezaji huyo wa Uingereza ametumwa ili kufanyiwa ukaguzi wa matibabu baada ya kulalamika kwamba ana uchungu katika sehemu ya wayo wake.

''Sielewi vyema kuhusu hali hii'',alisema mkufunzi wa klabu hiyo Jurgen Klopp.

Akizungumza baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Bordeaux kuisadia Liverpool kufuzu Klopp aliongezea:''Sio hali nilioona kwa sababu sisi hufanya mazoezi kwa makundi.Haikuwa karibu sana na mechi wakati tulipopata habari hizo.Kwa sasa'' itabidi tusubiri.