Robo fainali CECAFA kuanza leo

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya taifa

Michezo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji Cup itaanza kutimua vumbi leo huko Adis Ababa Ethiopia.

Timu ya taifa ya Uganda the cranes itakuwa dimbani kukabiliana na wanyasa Malawi , huku timu ya Tanzania bara maarufu kama The Kilimanjaro stars na Wenyeji Ethiopia.

Robo fainali ya pili itapigwa hapo jumanne Desemba mosi kwa Sudan kusini kukipiga na Sudan,Rwanda wakipepetana na Kenya.

Michezo ya nusu fainali itafanyika siku ya Alhamisi huku mchezo wa fainali na ule wa kumsaka mshindi wa tatu ikifanyika siku ya jumamaosi Desemba 5.