Rojo aumia bega mazoezini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marcos Rojo ni majeruhi hivyo atakaa benchi kwa wiki kadhaa

Beki wa Klabu ya Manchester united Marcus Rojo atakua nje ya uwanja kwa muda wiki kadhaa baada ya kuumia bega wakati wa mazoezi.

Ajalia hiyo ya kufanyatuka bega ilitokea wakati wa mazoezi ya Alhamis kwa bega lilelile lilofyatuka msimu uliopita katika mchezo dhidi ya Manichester City.

Rojo hakufanyiwa upasuaji kwa jeraha hilo ila alikaa nje ya dimba kwa muda wa wiki nne.

Klabu yake bado haijazungumzia swala la beki huyu ila ikitarajiwa kuwa leo ijumaa kocha mkuu wa kikosi hicho Louis van Gaal atazungumzia kuumia kwa beki huyo.

Beki huyo kisiki alisajiliwa mwaka 2014 akitokea timu ya Sporting Lisbon ya Ureno ya kwa dau la Pauni Milion 16, anaungana na beki mwingine wa kushoto Luke Shaw anayeuguza jeraha la kuvunjika mguu mara mbili .