Rooney kukosa mechi muhimu Man Utd

Rooney Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rooney hakumaliza mechi dhidi ya Leicester City

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney hatacheza mechi ya nyumbani dhidi ya West Ham Jumamosi na pia mechi muhimu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Wolfbsurg kutokana na jeraha.

Rooney anauguza jeraha la kifundo cha mguu.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 30 hakuweza kumaliza mechi waliyotoka sare 1-1 ugenini Leicester City wikendi iliyopita na atahitajika kusubiri muda zaidi kuchezea klabu hiyo mechi yake ya 500.

Meneja Louis van Gaal amesema tatizo hilo ni mbaya zaidi ya ilibyodhaniwa.

United wanahitajika kushinda mechi ya ugenini dhidi ya Wolfsburg Jumanne kujihakikishia nafasi hatua ya muondoano.

Difenda wa United Marcos Rojo naye ameumia kwenye bega.

Phil Jones na Ander Herrera kwa upande mwingine hawataweza kuchezea klabu hiyo dhidi ya West Ham, ingawa Jesse Lingard atarejea.