Leicester wachukua uongozi EPL

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

Leicester wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Uingereza baada ya kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Swansea. Arsenal, waliopata ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Sunderland wanashikilia nafasi ya pili wakifuatwa na Manchester City ambao wamekubali kulala 2-0 ugenini Stoke City.

Lecester wana alama 32, Arsenal 30, Man City 29 na Man Utd alama 29.

Msimamo wa ligi EPL
Namba Klabu Mechi Mabao Alama
1 Leicester 15 11 32
2 Arsenal 15 14 30
3 Manchester City 15 14 29
4 Manchester United 15 10 29
5 Tottenham 15 13 26
6 West Ham 15 4 23
7 Liverpool 14 3 23

Haya hapa matokeo kamili:

 • Stoke 2-0 Man City
 • Arsenal 3-1 Sunderland
 • Man Utd 0-0 West Ham
 • Southampton 1-1 Aston Villa
 • Swansea 0-3 Leicester
 • Watford 2-0 Norwich
 • West Brom 1-1 Tottenham
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manchester United wametoka sare 0-0 nyumbani dhidi ya West Ham

19:50 BAOOOO! Arsenal 3-1 Sunderland

Aaron Ramsey aongezea Arsenal la tatu muda ukielekea kumalizika.

19:50 BAOOO: Watford 2-0 Norwich

Bao la Odion Ighalo

19:38 Manchester United v West Ham

Martial anapata mpira eneo la hatari. Anambwaga kipa lakini pia anabwaga goli na mpira wake kuelekea nje. Manchester United wanaendelea kushambulia lakini bahati bado haijasimama.

Haki miliki ya picha AP

19:32 BAOOO! Southampton 1-1 Aston Villa

Oriol Romeu anasawazishia Southampton.

19:25 BAOOOO! Swansea 0-3 Leicester

Riyad Mahrez, anaongezea Leicester bao la tatu.

Haki miliki ya picha AFP

Haki miliki ya picha AP

19:20 BAOOOO! Arsenal 2-1 Sunderland

Dakika ya 63, Olivier Giroud, ambaye alijifunga kipindi cha kwanza kikikaribia kumalizika, anafungia Arsenal.

19:19 Manchester United v West Ham

Anthony Martial wa Manchester United anatamba, lakini anazuiwa kufunga na kipa Adrian. Muda mfupi baadaye, Alex Song anamfyeka Martial na inakuwa frikiki.

19:15 Manchester United v West Ham

Mauro Zarate wa West Ham anapata nafasi ya wazi, lakini anapiga mpira wake nje.

19:03 Mechi zinaanza tena, kipindi cha pili.

Ni muda wa mapumziko sasa

Mambo yako hivi mechi zinazoendelea

 • Arsenal 1-1 Sunderland
 • Man Utd 0-0 West Ham
 • Southampton 0-1 Aston Villa
 • Swansea 0-2 Leicester
 • Watford 1-0 Norwich
 • West Brom 1-1 Tottenham

18:45 BAOOOO! Arsenal 1-1 Sunderland

Olivier Giroud anajifunga na kusawazishia Sunderland muda wa mapumziko ukiendelea kukaribia.

18:43 Manchester United v West Ham

Morgan Schneiderlin anaumia na kuondoka uwanjani upande wa Manchester United, pengo analoacha linajazwa na Michael Carrick.

18:43 BAOOOO! Southampton 0-1 Aston Villa

Joleon Lescott anawapatia Villa bao la kwanza wakiwa ugenini St Marys.

18:41 Manchester United v West Ham

Victor Moses anaonekana kuumia. Anaondolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Michail Antonio.

18:40 BAAOOOO! West Brom 1-1 Tottenham

James McClean anasawazishia West Brom.

18:34 BAOOOO! Arsenal 1-0 Sunderland

Dakika ya 33, Arsenal wanajiweka kifua mbele kupitia Joel Campbell, ambaye amepokea pasi safi kutoka kwa Mesut Ozil.

Haki miliki ya picha AFP

18:32 BAOOO! Watford 1-0 Norwich

Watford wanafunga kupitia penalti inayochapwa na Troy Deeney baada ya Alex Tettey kumchezea visivyo Odion Ighalo.

18:27 Man Utd v West Ham

West Ham wanakaribia sana kufunga. Mauro Zarate anapiga mpira wa kichwa ambao unagongwa mlingoti wa goli, Winston Reid anarudisha tena mpira lakini unagonga mwamba wa goli.

Haki miliki ya picha AFP

18:21 BAOOOO: Swansea 0-2 Leicester

N'Golo Kante anampa pasi safi Riyad Mahrez ambaye hababaishi, anautuma mpira wavuni.

18:17 BAOOO! West Brom 0-1 Tottenham

Bao limefungwa na Dele Alli.

18:15 Man Utd v West Ham

Anthony Martial anapata mpira eneo la hatari. Kipa anamzuia kufunga, na inakuwa kona. Inapigwa lakini Man Utd hawafanikiwi.

18:11 Man Utd v West Ham

Kiungo wa West Ham Victor Moses anajipenyeza eneo la hatari. Kipa De Gea yuko macho na anamzuia kufunga.

18:05 BAOOOO! Swansea City v Leicester City

Riyad Mahrez anawapa Leicester bao la mapema, na kuwafikisha kileleni mwa msimamo wa ligi, kwa sasa. Anambwaga kipa Lukasz Fabianski kwa ustadi mkubwa.

18:04 Man Utd v West Ham

Marouane Fellaini anapata mpira pahala pazuri. Anawaangalia wenzake kisha kuamua kujaribu bahati. Kombora lake linaenda nje.

18:00 Mechi za mkumbo wa pili leo zinaanza.

Mechi hizo ni:

Arsenal v Sunderland Man Utd v West Ham Southampton v Aston Villa Swansea v Leicester Watford v Norwich West Brom v Tottenham

17:37 Mechi inamalizika Stoke City 2-0 Manchester City

Vijana wa Mark Hughes wanapata ushindi muhimu uwanja wa Britannia, mabao yote mawili yakifungwa na Marko Arnautovic.

Matokeo hayo yana maana kwamba City wanaweza kupitwa na timu tatu leo: Leicester City, Manchester United na Arsenal.

Haki miliki ya picha Reuters

17:35 Stoke City 2-0 Man City

Dakika ya 90, Raheem Sterling anajaribu bahati kutoka mbali bila mafanikio. Mechi imeongezwa dakika tatu.

2-0 17:27 Man Utd v West Ham

Anthony Martial ndiye atakayeongoza mashambulizi upande wa Manchester United lakini Memphis Depay amelishwa benchi. Matteo Darmian amepata nafasi safu ya ulinzi baada ya kuumia kwa Marcus Rojo.

West Ham ambao walimpoteza Diafra Sakho kutokana na jeraha watashambulia kupitia Andy Carroll. Alex Song anaanza mechi mara yake ya kwanza msimu huu.

17:22 Shakiri anatolewa uwanjani upande wa Stoke, na pahala pake anaingia Marco van Ginkel.

17:20 Dakika ya 76, Aleksandar Kolarov anapata nafasi nzuri upande wa Man City lakini anatikisa neti, kutoka nje.

17:18 Manchester City wanasalia 10 uwanjani baada ya Fernando kuumia na kutolewa nje ya uwanja. City walikuwa wametumia nafasi zao tatu za kubadilisha wachezaji. Jesús Navas alikuwa wa tatu akiingia nafasi ya David Silva.

17:15 Stoke City wamepoteza nafasi mbili nzuri za kufunga. Mambo bado yamesalia Stoke 2-0 Manchester City.

Manchester United v West Ham

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United XI: De Gea, Darmian, McNair, Smalling, Blind, Schneiderlin, Schweinsteiger, Mata, Fellaini, Lingard, Martial.

West Ham XI: Adrian, Tomkins, Reid, Ogbonna, Cresswell, Song, Noble (c), Kouyate, Moses, Zarate, Carroll

Arsenal v Sunderland

Arsenal XI: Cech, Mertesacker, Koscielny, Ozil, Giroud, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Monreal, Flamini, Bellerin, Campbell.

Benchi: Ospina, Debuchy, Gibbs, Gabriel, Walcott, Chambers, Iwobi.

Sunderland XI: Pantilimon, Yedlin, van Aanholt, Kaboul, O’Shea (nahodha), Coates, Toivonen, M’Vila, Watmore, Borini, Fletcher.

Benchi: Mannone, Rodwell, Gomez, Jones, Lens, Graham, Johnson.

17:00 City wanafanya mabadiliko mawili. Fabian Delph anaingia nafasi ya Fernandinho, Kelechi Iheanacho naye nafasi ya Wilfried Bony.

16:55 Stoke wanashambulia lakini kipa Hart anazimba kombora la kwanza. La pili kutoka kwa Marko Arnautovic linaenda nje.

16:50 Kipindi cha pili kinaanza. City wanaanza kwa kishindo, Sterling akishambulia.

16:33 Ni muda wa mapumziko sasa Stoke City 2- 0 Manchester City

Mabao ya Stoke yamefungwa na Marko Arnautovic

Haki miliki ya picha Reuters

16:28 Arnautovic nusura apate hat-trick. Anapata pasi nzuri na kubwaga walinzi wa City, kisha anambwaga kipa lakini kombora lake linagonga mlingoti na kurudi ndani uwanjani.

16:26 Aleksandar Kolarov anatoa kombora kali, lakini kipa wa Stoke yuko macho.

16:23 Erik Peters wa Stoke anatoa krosi safi kutoka kushoto, inamfikia Marko Arnautovic ambaye kombora lake linakosa goli pembamba.

16:17 Marko Arnautovic anapata mpira nafasi nzuri, badala ya kujaribu kulenga goli, anaurejesha nyuma kwa mwenzake lakini wachezaji wa City wanaunyakua.

16:15 De Bryune anakimbia na mpira lakini anakosa wa kumsaidia.

16:11 Raheem Sterling wa City ananawa mpira.

Haki miliki ya picha Reuters

16:10 Jack Butland anajaribu kupenyeza mpira eneo la hatari la Man City, lakini Marko Arnautovic ameshajenga kibanda ardhi ya wenyewe.

16:08 Furaha ya kufunga. Hapa ni Marko Arnautovic wa Stoke City akisherehekea baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Man City.

Haki miliki ya picha Reuters

16:03 Nicolás Otamendi wa Man City anajaribu kulipa deni baada yake kupokea pasi kutoka kwa David Silva. Lakini kombora lake linakosa lango.

16:00 BAOOOO! Stoke City 2-0 Man City

Bao limefungwa na Marko Arnuatovic. Kumbuka ndiye aliyefunga la kwanza.

Kumbuka Arsenal, Manchester United na Leicester watashuka dimbani saa kumi na mbili saa za Afrika Mashariki

15:59 Kevin de Bruyne anapata nafasi nzuri, lakini walinzi wa Stoke hawampi nafasi.

15:55 Erik Pieters wa Stoke anatupa mpira nje, na kuwa kona lakini Man City wanashindwa kuzalisha matunda.

15:52 Ibrahim Afellay (Stoke City) anafanya madhambi.

15:50 BAOOOO! - Stoke 1-0 Man City

Marko Arnautovic anafungua ukurasa wa mabao upande wa Stoke, akikamilisha shambulio maridadi kutoka kwa vijana wa Britannia. Krosi imetoka kwa Xherdan Shaqiri.

15:47 David Silva anaanza mambo akituma pasi kwa Bacary Sagna wingi ya kulia, lakini shambulio lao linazimwa na walinzi wa Stoke.

15:45 Mchezo unaanza uwanja wa Britannia. Stoke 0-0 Man City

15:43 Kabla ya mchezo kuanza, Man City ndio wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu Uingereza wakiwa na alama 29, wakifuatwa na Leicester ambao pia wana alama 29 lakini wanapungukiwa na mabao. Man City wataendelea kuvuna?

Haki miliki ya picha Reuters

15:40 Stoke XI: Butland, Pieters, Johnson, Shawcross, Wollscheid, Whelan, Cameron, Shaqiri, Arnautovic, Afellay, Bojan

Benchi: Haugaard, Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Diouf, Walters

15:40 Man City XI: Hart, Sagna, Otamendi, Demichelis, Kolarov, De Bruyne, Fernando, Fernandinho, Silva, Sterling, Bony

Benchi: Caballero, Navas, Kelechi, Delph, Garcia, Clichy, Humphreys

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kolarov amerejea kikosi cha kuanza mechi City

15:30 (Saa za Afrika Mashariki) Hujambo! Mechi za Ligi ya Premia zinaendelea leo Arsenal, Manchester United na Chelsea wote wakishuka dimbani, mechi ya mapema ikiwa Man City ugenini Stoke.

Mechi zinazochezwa leo ni (saa za GMT):

Stoke v Man City 12:45

Arsenal v Sunderland 15:00

Man Utd v West Ham 15:00

Southampton v Aston Villa 15:00

Swansea v Leicester 15:00

Watford v Norwich 15:00

West Brom v Tottenham 15:00

Chelsea v Bournemouth 17:30

Haki miliki ya picha Getty