Man Utd kukabiliana na Wolfsburg UEFA

Wolfsburg Haki miliki ya picha PA
Image caption Manchester United watakutana na klabu ya Wolfsburg kutoka Ujerumani

Michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) inatarajiwa kuendelea leo Desemba 8 kwa michezo kadhaa katika hatua ya makundi.

Real Madrid itakuwa ikichuana dhidi ya Malmo, Paris Saint-Germain watawakabili Shakhtar Donetsk zikiwa ni mechi za kundi A.

KUNDI: B:

PSV Eindhoven Wao watapepetana na CSKA Moscow, Wolfsburg watakuwa wakimenyana na Manchester United .

KUNDI: C:

Benfica watawakabili Atlético Madrid, na Galatasaray ya Uturuki itachuana na Astana

KUNDI: D:

Manchester City Watawakabili Borussia Mönchengladbach, huku Sevilla wao wakichuana na vijukuu vya bibi kizee vya Turin Klabu ya Juventus .

Na Desemba 9 kutapigwa mechi kadhaa katika mwendelezo wa michuano hiyo.

Mechi kwa ufupi (Saa za Afrika Mashariki):

Paris Saint Germain v Shakt Donetsk 22:45

Real Madrid v Malmö FF 22:45

VfL Wolfsburg v Manchester United 22:45

Man City v B Monchengladbach 22:45

PSV Eindhoven v CSKA Moscow 22:45

Benfica v Atletico Madrid 22:45

Galatasaray v FC Astana 22:45

Sevilla v Juventus 22:45