Benzema aondolewa timu ya taifa Ufaransa

Benzema Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Benzema huenda akakosa michuano ya Euro 2016

Karim Benzema amesimamishwa kutoka timu ya taifa ya Ufaransa hadi uchunguzi wa madai yanayohusiana na kanda chafu ya ngono ukamilishwe.

Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 27 sasa huenda akakosa fursa ya kucheza michuano ya ubingwa wa Ulaya yaani Euro 2016 ambayo Ufaransa ndiyo mwenyeji.

Benzema amesimamishwa kucheza na Shirikisho la Soka la Ufaransa.

Mshambuliaji huyo anachunguzwa kwa madai kwamba alihusika katika njama ya kutishia na kudai pesa kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Ufaransa Mathieu Valbuena.

Nyota huyo wa Real Madrid amekanusha madai hayo.