FA yamwadhibu Schweinsteiger mechi 3.

Chama cha soka cha England ( FA) kimetangaza kumfungia Kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger Mechi 3.

Kifungo hiki kinaanza mara moja baada ya Mjerumani huyo kuamua kutopinga Mashitaka yake kwa kosa ambalo Refa hakuliona na badala yake kuhukumiwa kwa ushahidi wa Mkanda wa Video.

Schweinsteiger yupo hatarini kufungiwa Mechi 3 baada ya kufunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka cha England, kwa kosa la la kinidhamu.

Schweinsteiger mwenye Miaka 31, anadaiwa kumpiga Beki wa West Ham Winston Reid kwa Mkono walipokuwa wakigombea Mpira wa Free kick katika kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika 0-0 J umamosi iliyopita.

Mwamuzi wa wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na Wachezaji wote Wawili baada ya tukio lenyewe.

Katika Taarifa yao, FA imesema kuwa tukio hilo lilipitiwa na waamuzi Watatu tofauti ambap o kila mmoja aliafiki kuwa lilistahili Kadi Nyekundu na ndio maana wakafungua Mashitaka dhidi ya Schweinsteiger.

Schweinsteiger atazikosa Mechi za Ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke City na kurejea kwenye Mechi na Chelsea.