TP Mazembe kukutana na Sanfrecce Hiroshima

Mazembe
Image caption Mazembe walishinda ubingwa Afrika kwa kulaza USM Alger ya Algeria

Mabingwa wa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakutana na timu ya Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan hatua ya robofainali fainali za Kombe la Dunia la Klabu Jumapili.

Washindi wa ligi ya Japan Sanfrecce Hiroshima wamelaza mabingwa wa Oceania Auckland City 2-0 leo kwenye mechi iliyochezewa Yokohama.

Mshindi wa mechi kati ya Mazembe na Hiroshima atakutana na mabingwa wa Amerika Kusini River Plate ya Argentina nusufainali Desemba 16.