Tyson Fury amevuliwa mkanda wa IBF

Image caption Tyson Furry akiwa na mikanda yake ya ubingwa

Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Tyson Fury amevuliwa mkanda wa IBF ikiwa ni chini ya wiki mbili baada ya kushinda.

Bondia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27, alitakiwa kukubali kupigana na Vyacheslav Glazkov ili kutetea mkanda huo lakini badala yake amekubali mchezo wa mruadiano dhidi ya Wladimir Klitschko.

Fury alimtandika Klitschko wa Ukraine kwa pointi Novemba 28 mwaka huu na kunyakuwa mikanda mitatu ya uzito wa juu iliyokuwa ikishikiliwa na bondia huyo.

Mwenyekiti wa IBF Lindsey Tucker amethibitisha taarifa hizo akidai kuwa Fury alipaswa kutetea kutetea mkanda huo kwa kuzichapa na Glazkov lakini badala yake ameamua kurudiana na Klitschko.

Fury ambaye hajapigwa katika pamano 25, amebakiwa na mikanda ya WBA na WBO wakati mkanda wa WBC ukiwa unashikiliwa na Deontay Wilder wa Marekani.