Mourinho:Tunapigania nafasi ya nne

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mourinho

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anataka kutimiza ndoto yake kwa kumaliza miongoni mwa timu nne bora mwishoni mwa msimu huu.

Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza,wako katika nafasi ya 14 wakiwa pointi 14 nyuma ya timu inayoshikilia nafasi ya nne.

''Pengine tuna fursa ya kufanikisha ndoto hii kwa kumaliza katika nafasi ya nne,ijapokuwa inawezekana lazima tujaribu'',alisema Mourinho.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea

Chelsea inaelekea kukabiliana na Leicester katika ligi kuu ya Uingereza.

Mchezo m'baya wa kilabu ya Chelsea's msimu huu umezua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo ,lakini Mourinho amesema ana hakika atasalia kuwa kocha Stamford Bridge.