TP Mazembe yachapwa 3 - 0 Klabu Bingwa Duniani

Image caption Wachezaji wa TP Mazembe

Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya kombe la dunia la vilabu timu ya Tp Mazembe imechapwa na wenyeji wa michuano hiyo timu ya Sanfrecce Hiroshima 3-0.

Wenyeji Hiroshima walipata mabao yao kupitia Tsukasa Shiotani, Dakika ya 44, Kazuhiko Chiba, 56, na Takuma Asano, akifunga bao la mwisho.

kipigo hicho kinainyima nafasi timu ya Tp Mazembe kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hivyo watachuana na Klabu America, ya Mexico, ambayo nayo ilichapwa kwa mabao 2-1 Guangzhou Evergrande.

Kwenye nusu fainali Sanfrecce Hiroshima, watawachuana na River Plate, huku Barcelona wakikipiga na Guangzhou Evergrande.