River Plate ya Argentina yatinga fainali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Timu ya River Plate

Timu ya River Plate, imekua timu ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la vilabu.

Miamba wa Argentina waliibuka kidedea mbele ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya Sanfrecce Hiroshima kwa kuichapa kwa bao 1-0.

Bao la ushindi la River Plate, lilifungwa na Lucas Alario, katika dakika ya 72 ya mchezo.

River Plate, wanasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali nyingine kati ya Mabingwa wa Ulaya Barcelona watakaokipiga na Guangzhou Evergrande.