Chelsea washinda, Man Utd walazwa nyumbani

Ivanovic Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ivanovic alifungia Chelsea bao la kwanza kipindi cha kwanza

Chelsea wamerejelea ushindi baada ya kulaza Sunderland 3-1 mechi yao ya kwanza bila Jose Mourinho aliyefutwa Alhamisi.

Uwanjani Old Trafford, mambo yamemwendea mrama meneja Louis van Gaal baada ya vijana wake wa Manchester Utd kukabidhiwa kichapo cha 2-1 na Norwich City.

Kwingineko uwanjani Goodison Park, Leicester wameendelea kushangaza ulimwengu wa soka kwa kukwamilia kileleni EPL kwa kulaza Everton 3-2.

Kufuatia kushindwa Jumamosi, Manchester United sasa wamo nambari tano kwenye jedwali wakiwa na alama 29 sawa na Spurs ambao wamo nambari nne lakini wanawazidi kwa magoli.

United wamo alama tisa nyuma ya Leicester walio kileleni wakiwa na alama 38. Nambari mbili na tatu zinashikiliwa na Arsenal (alama 33) na Manchester City (alama 32), klabu zote mbili zikikutana Jumatatu.

Matokeo kamili yalikuwa kama ifuatavyo:

 • Chelsea 3-1 Sunderland
 • Everton 2-3 Leicester
 • Man Utd 1-2 Norwich
 • Southampton 0- 2 Tottenham
 • Stoke 1-2 Crystal Palace
 • West Brom 1 -2 Bournemouth

19:54 Mechi zinamalizika

19:53 KADI NYEKUNDU kwa West Brom

Salomon Rondon wa West Brom anapewa kadi nyekundu. Sasa wanasalia tisa uwanjani.

19:52 Mechi nyingine inamalizika: Southampton 0-2 Tottenham

19:51 BAOOOO! Everton 2-3 Leicester

Kevin Mirallas anafungia Everton.

19:50 Mechi imemalizika Manchester Utd 1-2 Norwich City

19:49 Manchester United 1-2 Norwich City

Chris Smalling anajaribu bahati kwa kichwa lakini wapi. Mpira wake unaenda nje huku muda ukizidi kuyoyoma.

19:47 Everton 1-3 Leicester

Jamie Vardy anaondoka uwanjani akiwa amejishika paja. Ameumia?

Haki miliki ya picha Reuters

19:44 BAOOO! Stoke 1-2 Crystal Palace

Lee Chung-yong anaweka Palace mbele.

19:43 BAOOO! West Brom 1-2 Bournemouth

Bournebmouth wanapata penalti na kufungiwa na Charlie Daniels.

19:39 BAOOO!West Brom 1-1 Bournemouth

Gareth McAuley anasawazishia West Brom.

19:37 Chelsea 3-1 Sunderland

Loic Remy anaanza kazi mara moja akijipenyeza kulia kisha kutoa kombora ambalo linazuiwa na kipa Costel Pantilimon.

19:36 Chelsea 3-1 Sunderland

Diego Costa anaondolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Loic Remy.

19:34 BAOOO! Stoke 1-1 Crystal Palace

Bojan anasawazishia Stoke.

19:33 Manchester United wanaendelea kushambulia vikali Norwich.

19:31 BAOOO! Everton 1-3 Leicester

Leicester wanaendelea kutawala Goodison Park. Shinji Okazaki anawafungia la tatu. Amesaidiwa na Jamie Vardy.

19:28 Chelsea 3-1 Sunderland

Cesc Fabregas anaondolewa uwanjani na badala yake anaingia Jon Obi Mikel

19:25 BAOOO! Everton 1-2 Leicester

Riyad Mahrez anarejesha Leicester mbele kupitia penalti baada ya Tim Howard kumwangusha Jamie Vardy.

19:22 BAOOOO! Manchester United 1-2 Norwich City

Anthony Martial anakomboa moja upande wa Manchester United kwa guu la kushoto.

Haki miliki ya picha All Sport

19:20 Everton 1-1 Leicester

Goodison Park, mshambuliaji Jamie Vardy anapata mpira eneo la hatari, kombora lake linatoka nje.

19:16 Manchester United 0-2 Norwich City

United wanafanya badiliko la kwanza, LVG akimtoa Marouane Fellaini na kuingiza Ander Herrera.

19:15 West Brom 0-1 Bournemouth

Vijana 10 wa West Brom wanafungwa na Adam Smith wa Bournemouth.

Haki miliki ya picha Getty Images

19:13 BAOOOO! Chelsea 3-1 Sunderland

Kipa Thibaut Courtois anababaisha kutoka kwa mpira wa kichwa wa Younes Kaboul, na nguvu mpya anatinga bao Fabio Borini.

19:10 BAOOOO! Manchester United 0-2 Norwich City

Alex Tettey anaongezea Norwich la pili Old Trafford.

19:07 BAOOOO! Chelsea 3-0 Sunderland

Oscar anafunga penalti. Mashabiki bado wanaimba jina la Mourinho.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Oscar akisherehekea bao mechi ya awali

19:05 PENALTI Chelsea 2-0 Sunderland

Chelsea wanapata penalti baada ya Willian kuangushwa na kipa Costel Pantilimon. Alikuwa amepokea pasi kutoka kwa Pedro.

19:01 Chelsea 2-0 Sunderland

Sunderland wamefanya badiliko la pili wakiingiza mshambuliaji Fabio Borini nafasi ya Ola Toivonen.

19:00 Mechi zinaanza tena

18:47 NI WAKATI WA MAPUMZIKO SASA

 • Chelsea 2 0 Sunderland
 • Everton 1-1 Leicester
 • Man Utd 0-1 Norwich
 • Southampton 0-2 Tottenham
 • Stoke 0-1 Crystal Palace
 • West Brom 0-0 Bournemouth
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ivanovic alifungia Chelsea bao la kwanza

18:47 BAOOO!Stoke 0-1 Crystal Palace

Connor Wickham anafungia Palace kupitia penalti.

18:44 Chelsea 2-0 Sunderland

Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea wanaonekana kurejelea makali yao. Wameshambulia sana Sunderland.

18:44 BAOOO!Southampton 0-2 Tottenham

Dele Alli anaongezea Spurs bao la pili.

18:42 Southampton 0-1 Tottenham

Uwanjani St Marys,Harry Kane anaweka Spurs kifua mbele.

18:38 BAOOO! Manchester United 1-0 Norwich City

Cameron Jerome anawapiga chenga walinzi wa Man Utd kisha kumbwaga De Gea.

18:37 KADI NYEKUNDU West Brom 0-0 Bournemouth

West Brom wanasalia 10 uwanjani baada ya James McClean kuonyesha kadi nyekundu.

18:35 Chelsea 2-0 Sunderland

Sunderland nusura wakomboe moja lakini kombora la Duncan Watmore linaelekea nje.

18:32 BAOOOO! Everton 1-1 Leicester

Romelu Lukaku anasawazishia Everton.

Haki miliki ya picha z

18:29 BAOOOO! Everton 0-1 Leicester

Riyad Mahrez anafunga mkwaju wa penalti na kuweka viongozi wa ligi Leicester mbele.

18:28 PENALTI Everton 0-0 Leicester

Ramiro Funes Mori anamwangusha mchezaji wa Leicester down Shinji Okazaki.

18:27 Chelsea 2-0 Sunderland

Meneja wa Sunderland anamtoa Sebastian Coates na kuingiza Adam Johnson.

18:25 Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea wanaendelea kutawala. Costa, Oscar na Fabregas wanazomewa na mashabiki kila wanapopata mpira.

18:24 Man Utd wanaendelea kushambulia na kudhibiti mpira Old Trafford. Wanapata kona mbili za haraka lakini hazizai matunda.

18:18 Manchester United wanaendelea kushambulia. Juan Mata anapenya ngome ya Norwich, na kumpitishia mpira Rooney. Rooney anatoa kombora lakini wapi? Man Utd bado hawajafanikiwa kulenga goli.

18:13 BAOOO! Chelsea 2-0 Sunderland

Chelsea wanaongeza la pili kupitia Pedro. Krosi imetoka kwa Branislav Ivanovic upande wa kulia, mpira ukamgonga Sebastian Coates kabla ya kumfikia Pedro.

18:11 Man Utd 0-0 Norwich

Wayne Rooney anatumbukiza mpira wavuni lakini yeye, na mwenzake Marouane Fellaini walikuwa wameotea. Bao linakataliwa.

18:07 BAOOOO! Chelsea 1-0 Sunderland

Branislav Ivanovic, anaifungia Chelsea. Amefunga kwa kichwa baada ya kona kupigwa na Willian.

18:06 Everton 0-0 Leicester

Uwanjani Goodison, Everton wameanza vyema wakishambulia wageni wao, ambao kwa sasa wanaongoza jedwali.

18:03 West Brom 0-0 Bournemouth

Kipa wa West Brom Boaz Myhill anafanyishwa kazi mapema na Junior Stanislas anayetoa kombora kutoka mbali.

18:02 Guus Hiddink ameketi pamoja na Didier Drogba na Roman Abramovich.

Mashabiki wengi wamebeba mabango, wakimuunga mkono Mourinho.

Haki miliki ya picha PA

18:00 Mechi zinaanza

17:57 Wachezaji wanajiandaa kuingia viwanjani.

Mechi zinazoanza ni:

 • Chelsea v Sunderland 18:00
 • Everton v Leicester 18:00
 • Man Utd v Norwich 18:00
 • Southampton v Tottenham 18:00
 • Stoke v Crystal Palace 18:00
 • West Brom v Bournemouth 18:00

17:52 Meneja mpya wa Chelsea Guus Hiddink yumo Stamford Bridge, sawa na mmiliki wa klabu hiyo Guus Hiddink. Chelsea wanasimamiwa leo na Steve Holland.

17:47 Jose Mourinho, baada ya kufutwa kazi Alhamisi, leo amejitokeza na kwenda kushabikia mechi kati ya Brighton na Middlesbrough katika ligi ya daraja la pili Uingereza, ligi ya Championship katika uwanja wa Amex.

Kabla ya mechi hiyo Middlesbrough inaongoza ligi hiyo, ikifuatwa na Brighton kwa wingi wa mabao, timu zote mbili zikiwa sawa kwa alama 43. Mourinho ni rafiki wa meneja wa Middlesbrough Aitor Karanka.

Middlesbrough mwishowe wamechomoka na ushindi wa 3-0 na kufungua mwanya wa alama tatu kileleni kwa kufikia alama 46.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mourinho uwanjani Amex

Haki miliki ya picha PA

17:30 Mameneja wametangaza vikosi vyao. Upande wa Manchester United Wayne Rooney amerejea.

Man Utd v Norwich

Man Utd XI: De Gea, Young, Jones, Smalling, Blind, Carrick, Fellaini, Memphis, Mata, Martial, Rooney

Norwich XI: Rudd; Martin, Bennett, Bassong, Olsson; Redmond, O'Neil, Tettey, Brady; Hoolahan; Jerome

Everton v Leicester

Everton XI: Howard, Baines, Funes Mori, Stones, Coleman, Barry, Cleverley, Kone, Barkley, Deulofeu, Lukaku

Benchi: Joel, Gibson, Mirallas, Lennon, Besic, Osman, Galloway

Haki miliki ya picha Reuters

Leicester XI: Schmeichel, Simpson, Morgan, Wasilewski, Fuchs, Mahrez, Kanté, King, Albrighton, Okazaki, Vardy

Benchi: De Laet, Kramaric, Ulloa, Dyer, Benalouane, Schwarzer, Inler

Chelsea v Sunderland

Chelsea XI: Courtois; Ivanovic, Zouma, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Willian, Oscar, Pedro; Costa.

Benchi: Asmir Begović, Gary Cahill, Baba Rahman, Mikel, Ramires, Traore, Remy.

Haki miliki ya picha Other
Haki miliki ya picha Other

Sunderland XI: Pantilimon, Jones, Coates, Kaboul, O’Shea,Van Aanholt, M’Vila, Rodwell, Toivonen, Watmore, Defoe.

17:22 Habari kuu leo ni kuteuliwa kwa meneja wa zamani wa Uholanzi Guus Hiddink kuwa meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu. Jose Mourinho alifutwa kazi Alhamisi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hiddink aliongoza Chelsea kushinda Kombe la FA 2009

17:20 Hujambo, karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu mechi za Ligi ya Premia.

Ligi inarejelewa leo kwa mechi saba, Chelsea wakicheza mechi ya kwanza bila Mourinho, Man Utd nao wakiwa nyumbani dhidi ya Norwich.

Haki miliki ya picha Getty

Mechi zinazochezwa leo ni:

 • Chelsea v Sunderland 18:00
 • Everton v Leicester 18:00
 • Man Utd v Norwich 18:00
 • Southampton v Tottenham 18:00
 • Stoke v Crystal Palace 18:00
 • West Brom v Bournemouth 18:00
 • Newcastle v Aston Villa 20:30