Barcelona ndio klabu bingwa 2015

Image caption Barcelona ndio mabingwa wa dunia wa 2015 wa kombe la klabu bingwa.

Barcelona ndio mabingwa wa dunia wa 2015 wa kombe la klabu bingwa.

Mabingwa hao wa Uhispania waliibuka washindi baada ya kuilaza River Plate 0-3 katika fainali.

Ushindi huo ulikuwa wao wa 5 msimu huu

River hawakuwa na jibu kwa maswali yaliyoulizwa mbele ya lango lao na washambulizi wa Barca Luis Suarez, Lionel Messi na Neymar.

Messi ndiye aliyefungua kichapo hicho kunako dakika ya 36'' ya kipindi cha kwanza.

Licha ya kuwa alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu arejee kutoka hospitalini alikokuwa anatibiwa maradhi ya figo, rai huyo wa Argentina alifuma mkwaju wa Neymar.

Punde baada ya mapumziko Luiz Suarez alitumia vyema pasi nzuri kutoka kwa Sergio Busquets na kufanya mambo kuwa 2-0 kwa vigogo hao wa soka ya Uhispania.

Image caption Kufikia sasa the Catalans wametwaa mataji 5 kati ya sita wanazowania msimu huu.

Suarez hakuachia hapo alihakikishisia Barca ushindi alipotikisa wavu kunako dakika ya 68.

Bao hilo la pili lilimpa mshambuliaji huyo machachari wa Uruguay mabao 5 katika mechi mbili baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa nusu fainali dhidi ya Guangzhou Evergrande.

Kufikia sasa the Catalans wametwaa mataji 5 kati ya sita wanazowania msimu huu.

Kwa sasa wanaongoza jedwali la ligi ya Uhispania,,wanawania raundi ya 16 bora katika mechi za kombe la mfalme , Copa del Reyna ligi ya mabingwa barani Uropa.

Barcelona wamefunga mabao 176 msimu huu