Watford yatoa onyo Ligi kuu England.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mafahali wawili walipomenyana.

Ligi kuu ya soka ya England imendelea tena hapo jana kwa michezo miwili ,ambapo Watford waliwaalika Liverpool na matokeo ni kwamba Watford imechomoza na ushindi mnono wa mabao 3-0 ambayo yamefungwa na wachezaji Nathan Aki pamoja na Idion Ighalo akifunga mabao 2 , likiwa ni bao la 12 kwa mchezaji huyo katika msimu huu.

Katika mchezo mwingine swansea dhidi ya West Ham ni kwamba mchez huo ulimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya bila kufungana (0-0) .

Ligi hiyo itaendelea tena kwa mchezo mmoja ambapo Arsenal watakuwa nyumbani Emirate wakiwakaribisha Manchester City.

Real Madrid imeiadhibu Rayo kwa mabao 10-2 La Liga.